DR. STEPHEN MUNGA |
Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, ambaye pia ni Chancellor wa Sebastian Kolowa Memorial University{SEKOMU} Dr. Stephen Munga awataka wakristo nchini kuwa na uvumilivu na kutokulipiza kisasi hasa katika kipindi hichi cha mgogoro baina ya wakristo na waislamu.
Akiongea katika ibada ya kufungua mwaka wa 6 wa masomo katika chuo kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa,{SEKOMU} Mapema leo asubuhi tarehe 22 mwezi wa 10 chuoni hapo, aliwataka wakristo nchini kuwa wavumilivu na kutokulipiza kisasi kwa matukio ya uchomaji wa makanisa yaliyotokea hivi karibuni huko mbagala Jijini Dar es salaam tukio lililosababishwa na waumini wa dini ya kiislamu.
Akitoa mifano kwa umakini mkubwa kutoka karne ya 3 na karne ya 4, Askofu Munga alisema ,
" KULITOKEA VITA VYA KUPINGA UKRISTO NA KUUFUTA KABISA, WALICHOMA BIBLIA ILI KUUMALIZA UKRISTO LAKINI UKRISTO MPAKA LEO UPO"
Akiendelea kuwapa moyo wakristo Askofu Munga alisema
" WANAWEZA KUCHOMA BIBLIA ZOTE, WANAWEZA WAKACHOMA MAKANISA YOTE, LAKINI HATUTATETEREKA KWA SABABU NENO LA MUNGU LIKO MIOYONI MWETU"
Alionekana kusema maneno haya kwa uchungu huku akiukumbuka mchango na wosia wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Aidha Askofu Munga, alisisitiza swala la kutendeka kwa haki nchini kwa kuwataka viongozi wenye madaraka kuyatumia madaraka yao vema kwa manufaa ya jamii nzima na kusema matatizo yote lazima yatatuliwe kisheria huku akipinga msemo wa
"AMANI HAIJI ILA KWA NCHA YA UPANGA"
na kusisitiza kuwa majivu ya makanisa yaliyochomwa ni ishara ya kuzaliwa kwa Tanzania mpya yenye Amani ya kweli.