TUMAINI UNIVERSITY MAKUMIRA
P.O. BOX 370 , Lushoto.
Email: tumasosekuco@gmail.com
ZABUNI YA KUENDESHA CAFTERIA YA WANACHUO
KWA MWAKA 2012/2013
Sebastian Kolowa
University College ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini University.Chuo hiki
kipo umbali wa kilomita nane kaskazini
mwa mji wa Lushoto, Barabara kuu iendayo Mlalo , katika safu za milima ya
kijani kibichi ya Usambala kwa jina la utani ; Uswisi ya Afrika;
Chuo Kikuu kinakaribisha ZABUNI ya kuendesha Cafteria ya wanachuo.
Cafteria hii inauwezo wa kuhudumia watu wasiopungua 600 kwa wakati mmoja.
Sifa za mwombaji;
(a) Awe na leseni ya kuendesha Cafteria/Hoteri/Mgahawa.
(b)
Awe na VAT na
TIN. Aonyeshe uwezo wa kifedha
(c) Awe na uzoefu wa kuendesha Cafteria/Hoteri/Mgahawa kwa
muda usiopungua miaka mitatu au zaidi.
(d)
Ataje kiwango cha
kodi atakacholipa kwa mwezi. Cafteria inavifaa muhimu kama
vile meza, viti,meza za maandalizi na vyumba baridi vya kuhifadhia vyakula
mbalimbali.
(e) Ataje aina ya majiko atakayotumia Kwa kupikia kama vile Gesi Umeme au Mkaa.
(f) Aainishe aina za vyakula na bei zake.
(g)Awe
na vifaa vya msingi kama vile sahani, bakuli,
glasi, vikombe, vijiko, umma, visu n.k.
MASHARTI
YA ZABUNI;
(a)
Maombi
yaliyofungwa vizuri Kwa Lakiri na kuandikwa juu ya bahasha ‘ZABUNI YA KUENDESHA CAFTERIA YA WANACHUO’na kupelekwa kwa katibu,
Serikali ya Wanachuo TUSO – SEKUCo,
S.L.P 370, Lushoto.
(b)
Mwombaji
anatakiwa kulipa ada ya zabuni ya Tshs. 50,000/= (Elfu hamsini) tu, fedha
ambayo hairudishwi.Zabuni iambatane na pay- in – slip ya malipo hayo,
itakayolipwa kupitia, SEKUCo –SO. A/C No.
4162301220 NMB Lushoto Branch.
(c)Mwombaji ataruhusiwa kutembelea Cafteria hiyo siku za
kazi kuanzia saa 2.30 asubuhi hadi saa10.30 jioni.
(d)
Mzabuni
atatakiwa kuonyesha aina ya vyakula na bei zake.
(e)Siku ya mwisho ya kuleta zabuni itakuwa tarehe 14 Julai 2012 saa 4.00 asubuhi.
(f)
Zabuni
zitafunguliwa mbele ya wazabuni walioomba au wawakilishi wao kwenye ufunguzi
huo tarehe 14 Julai 2012 saa 4.00
asubuhi.
(g)
Muombaji
atakayefanikiwa ataruhusiwa kuendesha Cafteria husika.
Kwa mawasiliano zaidi piga
namba zifuatazo;
+255 7131 29097.
+255 7543 60761.
+255 7547 65515.
Katibu
SERIKALI YA WANACHUO TUSO –SEKUCo
S . L . P 370, LUSHOTO.