.

.

.

.


TUMSIFU THE GREAT

BEHIND THE SCENE

  • MOVIE SHOOTING

    Wakati wa utengenezaji wa movie inayoitwa BACK TO SCHOOL
  • BACK TO SCHOOL

    SHOT IN TANGA TANZANIA
  • MUSIC VIDEO

    Wakati wa utengenezaji wa music video inakwenda kwa jina la I NEED U
  • MOVIE BACK TO SCHOOL

    Directed by TUMSIFU KOMBE
  • BACK TO SCHOOL

    wakati wa utrngenezaji wa movie inayoitwa BACK TO SCHOOL
  • MOVIE NAME-WIVU

    Behind the scene ya upigaji picha wa movie inayoitwa WIVU
  • MUSIC VIDEO HERE

    Upigaji wa picha wa Music video, msanii anajulikana kwa jina la Rider, wimbo DECEMBER, Shot in Tanga Tanzania
  • MOVIE-WIVU HERE

    Upigaji picha wa movie inayojulikana kwa jina la WIVU

Monday, June 4, 2012

MASHINDANO YA INTERCOLLEGE LUSHOTO YAFANA, SHETA AFUNIKA MBAYA!


Mashindano ya intercollege yaliyoandaliwa na five entatainment wilayani  lushoto yakivihusisha vyuo vitatu ambavyo ni Tumaini University ( SEKUCO) Chuo cha uongozi wa mahakama IJA na Chuo cha CDTTI mabughai. Mashindano hayo yaliyoanza tarehe 2 na kumalizikia tarehe 3 ambapo kulikuwa na mashindano ya kumsaka miss na super model usiku ndani ya Ukumbi wa CCM hall ambapo Msani Shetta wa da stamina aliwakonga mashabiki wake kwa kupiga shoo ya kufa kiumbe


                        UFUNGUZI WA MASHINDANO TAR.2 JUNE

Mashindano yalifunguliwa  na katibu mkuu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo ambapo mchezo wa netball ulianza dhidi ya timu ya netball SEKUCO na timu ya netball CDTTI mabughai. katika mashindano hayo timu ya SEKUCO iliibuka kidedea kwa kuichapa timu ya CDTTI mabughai na kujinyakulia ushindi

mfungaji wa timu ya sekuco akimimina magoli ya kutosha kwa upande wa timu ya CDDTI Mabughai

                                      MASHINDANO   YA VOLLEYBALL

Vijana machachari wa timu ya volleyball ya chuo kikuu cha Sebastian Kolowa, waliwachapa wapinzani wao magoli mengi tuuuuuu tena ya kutosha, hatimaye wapinzani wao hao chuo cha CDTTI Mabughai wakaibuka washindwa katika mechi hiyo kwa kulishwa set nyingi tuu.

kikosi cha timu ya volleyball sekuco



  
                                        MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU 

Mpira wa Miguu ulianza kwa mchuano kati ya club mbili zilipo chuoni hapo ambazo ni JIMWAGE FC na LA-KUCHUMPA FC, katika mchuano huu mkali timu ya JIMWAGE FC kupitia streka wake Kasumuni waliwachapa wapinzani wao hao wa jadi kwa kupitia penalt.
STREKA WA KULIPWA WA JIMWAGE FC AKISHANGILIA BAADA YA KUWALAMBA LA-KUCHUMPA FC BAO KWA KUPITIA PENALT

FULL SHANGWE KWA WACHEZAJI NA MASHABIKI WA JIMWAGE FC



 WANA-JIMWAGE FC WAKIENDELEA KUSASAMBUA KWA USHINDI WALIOUPATA DHIDI YA VIBONDE WAO LA-KUCHUMPA FC  
                         
  

MPIRA WA MIGUU KATI YA TIMU YA SEKUCO NA                 TIMU         YA    CDTTI MABUGHAI

  Timu ya mpira wa miguu ya chuo cha Sekuco pia waliibuka washindi dhidi ya timu ya chuo cha CDTTI Mabughai kwa kuwachapa bao 3-1.
Kikosi cha SEKUCO
  



MASHABIKI WAKIENDELEA KUSHANGILIA HUKU WAKILA KWAITO LIVE LIVE





HAYA SASA YOTE TISA, KUMI NI HAPO CCM HALL AMBAPO PALIKUWA NA PATASHIKA LA KUMSAKA MISS NA SUPER MODEL KWA VYUO HIVI VITATU

Mashindano hayo yalifanyika kwa ushabiki mkubwa huku kukisindikizwa na shoo kali kutoka kwa mkali wa mdananda SHETA da stamina, ambapo majaji walikuwa na kazi ngumu kumpata mshindi kutokana na jinsi washiriki walivyokuwa wamejiandaa.
kwa upande wa super   models mshindi wa kwaza alitoka chuo cha CDTTI mabughai akifuatia na mshindi toka chuo cha SEKUCO na Mshindi wa Tatu pia alitokea chuo cha SEKUCO.
Kwa upande wa Mamiss mshindi wa kwanza mpaka watatu walitoka chuo cha Uongozi wa mahakama IJA


washiriki waonesha ujuzi jukwaani




MSHIRIKI NDANI YA VAZI LA UBUNIFU


MASHABIKI





THE GREAT HIMSELF AKIRECORD MATUKIO
SHETA AKIMWAGA SUMU JUKWAANI


 





ALIYESIMAA MWENYE KOTI JEUSI NI MPIGA PICHA WA KAMPUNI YA TUMSIFU THE GREAT FILM PRODUCTION BWANA SANGA TS





 
PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILI ZITAKUJIA PUNDE

SPECIAL THANX TO MATUTA BARNABA.

RIDER_DECEMBER OFFICIAL VIDEO, VIDEO DIRECTED BY TUMSIFU KOMBE THE GREAT

CHAZ MAVOKO-SONG KWAHERI, Video directed by Tumsifu the great films

wibiya widget

TUMSIFU THE GREAT © 2012.All Rights Reserved.Designed by Tumsifu Kombe Modified by Nicolaus Trac-0716 276 000 :ICT EXPERT Sponsored by: JIPANGE