Chuo kikuu kishiriki cha Tumaini university makumira, Sebastian Kolowa university College (SEKUco)kilichopo mkoani Tanga kimetoa elimu ya uraia kwa shule,na wananchi wilayani Lushoto.
Sebastian Kolowa university College (SEKUco) ambacho ni chuo pekee Tanzania kinachotoa Shahada ya Elimu ya mahitaji maalumu, Shahada ya Sheria pamoja na Shahada na Eco-tourism na Nature Conservation kilitoa elimu hiyo jana 10/05/2012 kwa Kuanzia na Shule ya sekondari Magamba iliyopo wilayani Lushoto
Kupitia Organisation iliyoanzishwa Chuoni hapo na wanafunzi wanaosoma Elimu ya Siasa na Uongozi (political science and Public Adminstration) ijulikanayo kama SEPSSA ( Sekuco Political Science Student Association) walitoa elimu ya Uraia kwa Wanafunzi wa Shule hiyo kuhusiana na maswala ya haki na wajibu wa raia, uchaguzi huru na wa haki, na kujibu Maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wanafunzi hao-
WANAFUNZI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA |
Akifungua warsa hiyo Mwenyekiti wa SEPSSA Sande Salum, ambaye ni mwanafunzi wa Shahada ya Elimu Maalumu, Sayansi ya Siasa na Uongozi (POLITICAL SCIENCE NAD PUBLIC ADMINSTRATION) aliwasihi wanafunzi hao kuzielewa haki zao za kimsingi pamoja na kuwajibika kwa faida yao na Taifa kwa ujumla, Huku akiwaelezea umuhimu wa Rasilimali zilizoko wilayani kwako ikiwa ni pamoja na misitu na mazao mbalimbali ya chakula na matunda pia.
MWENYEKITI WA SEPSSA AKIWASILISHA MADA |
MHAMASISHAJI TEDDY SANGA AUGUSTINO |
KUTOKA KUSHOTO, HEADMASTER WA MAGAMBA SECONDARY. 2, MWALIMU 3. MJUMBE WA SEPSS, SANGA TEDDY AUGUSTINO, 3. MWENYEKITI WA SEPSSA MR. SANDE SALUM |
"SEPSSA FOR CHANGE"