.

.

.

.


TUMSIFU THE GREAT

BEHIND THE SCENE

  • MOVIE SHOOTING

    Wakati wa utengenezaji wa movie inayoitwa BACK TO SCHOOL
  • BACK TO SCHOOL

    SHOT IN TANGA TANZANIA
  • MUSIC VIDEO

    Wakati wa utengenezaji wa music video inakwenda kwa jina la I NEED U
  • MOVIE BACK TO SCHOOL

    Directed by TUMSIFU KOMBE
  • BACK TO SCHOOL

    wakati wa utrngenezaji wa movie inayoitwa BACK TO SCHOOL
  • MOVIE NAME-WIVU

    Behind the scene ya upigaji picha wa movie inayoitwa WIVU
  • MUSIC VIDEO HERE

    Upigaji wa picha wa Music video, msanii anajulikana kwa jina la Rider, wimbo DECEMBER, Shot in Tanga Tanzania
  • MOVIE-WIVU HERE

    Upigaji picha wa movie inayojulikana kwa jina la WIVU

Saturday, May 4, 2013

MWANACHUO IFM AUAWA KWA CHAKULA CHA SUMU


          Habari  toka chuo cha usimamizi wa fedha,  IFM- Dar es salaam  ni  kwamba  mwanafunzi  mmoja ambaye  bado  hatujafanikiwa  kulipata  jina  lake  amefariki  dunia  kwa  kulishwa  sumu  katika  chakula  alicholetewa  na  mpenzi  wake  ambaye  ni  mke  wa  mtu


          Taarifa  zaidi  zinadai  kwamba Mwanafunzi huyo alikuwa na uhusiano wa karibu sana na mke  wa mtu  ambaye  mbali  na  starehe  za  kimapenzi  alikuwa  pia  anampekea  chakula  cha  jioni


Baada ya  mchezo  huo  kudumu  kwa  muda, mume wa  mwanamke  aliusoma  mchezo  mzima  na  kuandaa  tego  la  kuwaangamiza  wote.


           Habari  zinadai  kwamba  Siku ya jumatano jioni mwanaume  huyo aliwahi  kurudi  nyumbani   na  kufanikiwa  kukinasa  chakula  kilichokuwa  kimeandaliwa  tayari  kwa  kupelekwa  kwa  huyo  mwanafunzi  ambaye  alikuwa  anatembea  na  mke wake.....


Baada  ya  kukinasa, alijifanya  kuzuga  na  kupotezea...Mkewe  alipotoka  alikichukua  na  kukitia  sumu  chakula  hicho  na  kisha  kukiweka   kama  kilivyokuwa  kimeandaliwa


              Inadaiwa Lengo  lake  lilikuwa   ni  kuwamaliza  wote  maana  alijua  ni  lazima  akifika  watakaa na kula  pamoja.

              Mwanamke alipopeleka chakula  hakukaa  kula  na  badala  yake   alimwambia yule mwanafunzi   kuwa  mume wake amewahi kurudi siku  hiyo  hivyo  hatoweza  kukaa  wale  pamoja....Mwanafunzi  huyo  akakipokea  na  kukila  na  ndipo  mauti  yakamkuta 



              Habari  toka  chuoni  hapo  zinadai  kwamba  mwanafunzi  huyo  alikuwa  ameshadisco  lakini  alikuwa  amepewa  nafasi  nyingine  ya  kurudia  mwaka  wa  pili , hivyo aliendelea kukaa mtaani kama mwanafunzi.



              Mwili wa marehemu bado uko Muhimbili kwa uchunguzi zaidi baada ya polisi kuuzuia kuzikwa....


Hizi  ni  habari  mbaya  sana  kwa  wanafunzi  wa  chuo  hicho maana ni jumatatu  tu  mwanafunzi mwingine  alifariki  katika  hali  ya  kutatanisha baada ya  kifo cha mpenzi  wake   miezi  michache  iliyopita.

           Habari za ndani zaidi zinadai   kuwa toka  mwaka  huu  uanze  mpaka sasa chuo  cha IFM  kimepoteza wanafunzi 12.

RIDER_DECEMBER OFFICIAL VIDEO, VIDEO DIRECTED BY TUMSIFU KOMBE THE GREAT

CHAZ MAVOKO-SONG KWAHERI, Video directed by Tumsifu the great films

wibiya widget

TUMSIFU THE GREAT © 2012.All Rights Reserved.Designed by Tumsifu Kombe Modified by Nicolaus Trac-0716 276 000 :ICT EXPERT Sponsored by: JIPANGE