TUMSIFU THE GREAT FILMS ni kampuni ya upigaji wa picha za video, inayojishughulisha na utengenezaji wa music videos, movies, documentary na matangazo mbalimbali.
TUMSIFU KOMBE (THE GREAT) ambaye ndiye mmiliki na Director wa kampuni hii na mwanafunzi katika chuo kikuu cha kumbukumbu ya Sebastina Kolowa ( SEBASTIAN KOLOWA MEMORIAL UNIVERSITY- SEKOMU) kilichopo mkoani Tanga, Amesema wako mbioni kuitoa filamu mpya, iliyosheheni wasanii wenye uwezo mkubwa kutoka Usambara Arts Groups
 |
ZOEZI LA UPIGAJI PICHA ZA FILAMU HIYO LIKIENDELEA |
Meck Kungulwi, Ambaye ni Mtunzi wa Story hiyo, Alisema filamu hiyo inayokwenda kwa jina la MDHAMINI, imetungwa kwa ustadi mkubwa na kuchezwa kwa ufanisi wa hali ya juu. Aidha aliongeza kuwa filamu hiyo imesheheni mfuatano wa mikasa ya kusisimua, kusikitisha na mikasa ya kimapenzi Pia kutakuwepo na Star wa Movie ya QUEEN MOMBO,ambaye pia ni msanii wa muziki, SHILOLE.
FILAMU HIYO ITAKUWA MADUKANI MUDA SI MREFU