![]() |
RAILA ODINGA |
Mgombea wa Urais Kenya Raila Odinga amepinga matokea ya Uchaguzi
yaliyotangazwa leo na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo na kuyaita matokeao
ya njama yaliyopangwa makusudi kuvuruga uchaguzi wa Urais Kenya.
Kutokana na matokeo yaliotangazwa leo na tume ya uchaguzi ya kumpa
ushindi Uhuru Kenyatta aliwashukuru wapiga kura kwa kujitokeza kwa
wingi na aliishutumu tume kwa kushindwa kufanya maamuzi ya haki na
kufanya madudu katika kuhesabu kura.
Aliendelea kusema serikali imetumia mamilioni kununua vifaa vya kisasa
vya kuandikisha na kuhesabia kura lakini cha ajabu vifaa vilishindwa
kufanya kazi na kusababisha kura kuhesabiwa upya kitu kilichofanywa kwa
makusudi ili kupanga matokeo. Kamwe mimi na wafauasi wangu
hatukubaliani na matokea na ili haki itendeke tutaelekea mahakamani na
alimalizia kwa kusema mvumilivu ula mbivu kwa hiyo ndugu zangu
tuvumilie tusubili maamuzi ya mahakama.