Jenista Mhagama Naibu Waziri wa Elimu Mafunzo na Ufundi |
Awali mwaka jana mwishoni, Naibu waziri anayeshughulikia Elimu (TAMISEMI),Kassim Majaliwa,alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari na kusema ajira hizo zinategemewa kutoka mwezi wa kwanza 2014,ambapo kauli hiyo haikutimia mpaka sasa mwezi wa pili na hakutoa tena tamko lolote juu ya hilo.
Mwishoni wa mwezi wa kwanza katibu wa Elimu Mafunzo na Ufundi, Prof. Sifuni Mchome,naye alitoa taarifa kupitia kituo kimoja cha TV,yaani EATV,akisema kila kitu tayari na wanasubiri kutangaza tu hizo ajira mpya za walimu,ambapo mpaka sasa pia kauli hiyo bado haijatimia maana ni kama wiki tatu zimeshapita.
Tarehe 11/02/2014,kulikuwa na kikao ambacho kilihusisha wadau mbalimbali wa elimu yaani walimu na wadau wengine wa sekta hiyo.Kikao hicho kiliendeshwa ndani ya ukumbi wa shule ya sekondari ya Lugalo iliyopo manispaa ya Iringa.
Kikao hicho ambacho mgeni rasmi alikuwa mh. Jenista Mhagama kama naibu waziri Elimu,aliweza kusikiliza mengi yanayoikumba sekta ya elimu.Pamoja na mambo mengi yaliyozungumziwa,wadau walitaka kufahamu ajira mpya za walimu zitatoka lini.
Kwa mujibu wa naibu waziri huyo alisema kuwa wale wote wanaosubiri ajira hizo,majina yatatoka tarehe 1/04/2014 kwasababu kwa sasa serikali haina fedha na nyingi zimetumika kwenye maswala mbalimbali ya kitaifa lakini kubwa ni maswala ya katiba mpya.
Kwa maelezo zaidi unaweza ukawasiliana na mdau yeyote wa elimu aliyehudhuria kikao hicho cha tarehe 11/02/2014,shule ya sekondari Lugalo iliyopo manispaa ya Iringa mjini.