Kuna taarifa kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper Mangweir ni kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia leo.
Hussein Original ambaye yupo Pretoria amesema Ngwear na M to the P ambaye walikuwa room moja wamekutwa wamezima baada ya kuzidhisha madawa ya kulevya...
Hata
hivyo mwenyeji wa rapper Albert Mangwea aliyefariki leo jijini
Johannesburg nchini Afrika Kusini, amesema hit maker huyo wa Mikasi
amefariki akiwa usingizini.
Akiongea muda mfupi uliopita, mwenyeji huyo aitwaye Jonathan amesema usiku wa kuamkia leo Mangwair alirudi nyumbani alikofikia akiwa mzima wa afya lakini mpaka kunakucha hakuonesha dalili za kuamka.
Ameongeza kuwa asubuhi kulipokucha aliondoka na kuendela na mishemishe yake na alipokuwa huko wenzake walimpigia simu kumtaarifu kuwa wamempeleka hospitali ya St. Helen ya jijini humo kwakuwa alikuwa bado hajaamka na ndipo walipogundua kuwa ameshafariki.
Jonathan amesema hakuweza kujua sababu za kifo cha Ngwair kwakuwa maelezo ya daktari yalikuwa kitaalam kiasi cha kushindwa kuelewa. Ngwair alikuwa amepanga kurudi leo nchini.
Taarifa za kifo cha Ngwair zimepokelewa kwa mshtuko na watu na makampuni mbalimbali nchini yametuma salamu za rambi rambi kupitia kwenye mitandao ya kijamii.
Kilimanjaro Lager
Umeondoka wakati bado tasnia ya muziki inakuhitaji. Pumzika kwa Amani Albert Mangwea “Cowwizy”.
Ndovu Special Malt
R.I.P Albert Mangweir! You will be missed by many Tanzanians.
Adam Nditi
Yani siamini Mangwear amefariki dunia nini ilichomkuta #RIP #Mangwair #akaCowbama
Diva
Jamani Ngwair , am in tears now ….. Jamani!. I can’t believe this. I can’t tweet The RIP….. Whyyyyy?
SOURCE.freebongo