.

.

.

.


TUMSIFU THE GREAT

BEHIND THE SCENE

  • MOVIE SHOOTING

    Wakati wa utengenezaji wa movie inayoitwa BACK TO SCHOOL
  • BACK TO SCHOOL

    SHOT IN TANGA TANZANIA
  • MUSIC VIDEO

    Wakati wa utengenezaji wa music video inakwenda kwa jina la I NEED U
  • MOVIE BACK TO SCHOOL

    Directed by TUMSIFU KOMBE
  • BACK TO SCHOOL

    wakati wa utrngenezaji wa movie inayoitwa BACK TO SCHOOL
  • MOVIE NAME-WIVU

    Behind the scene ya upigaji picha wa movie inayoitwa WIVU
  • MUSIC VIDEO HERE

    Upigaji wa picha wa Music video, msanii anajulikana kwa jina la Rider, wimbo DECEMBER, Shot in Tanga Tanzania
  • MOVIE-WIVU HERE

    Upigaji picha wa movie inayojulikana kwa jina la WIVU

Sunday, December 11, 2011

SIKU NILIYOTEMBELEA IRENTE CHILDRENS`s HOME MIMI PAMOJA NA SEDO ORGANISATION-TUMAINI UNIVERSITY





  Ni siku ya jumamosi tarehe 10 dec 2011 ambapo wanachuo walioko ndani ya jumuiya ya  SEDO ( Special Educators for Disabled and Orphans)  kutoka chuo kikuu cha SEBASTIAN KOLOWA UNIVERSITY COLLEGE OF TUMAINI UNIVERSITY TANGA, ilipoamua kukitembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha IRENTE CHILDREN`S HOME { ICH} kinachomilikiwa na KKKT dayosisi ya kaskazini kilichopo mkoani Tanga Wilayani lushoto.
     Wana SEDO Hao ambapo miongoni mwao wanasomea Shahada mbalimbali chuoni hapo ikiwepo shahada ya elimu maalumu (SPECIAL NEEDS EDUCATION) Ambapo ndani yake kuna wanachuo wenye uwezo wa kuwahudumia watoto wenye matatizo mbalimbali kama wenye matatizo ya uoni, wasiosikia, matatizo ya akili, matatizo ya kuongea. Wanajumuiya hao walichangia

michango yao kwa dhati kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaolelewa katika kituo kicho cha kulelea watoto yatima. Michango yao iliambatana na kufanya kazi mbalimbali kituoni hapo kama vile kuchanja kuni na kuosha vyombo ikiwa ni pamoja na kuonana na watoto hao. Wanachuo hao walipokelewa na viongozi mbalimbali chuoni hapo akiwemo Mrs Joyce Kibanga, ambaye ni mkurugenzi wa huduma za jamii wilayani humo.


UFUATAO NI MTIRIRIKO WA BAADHI YA PICHA NA MAELEZO MAFUPI  ZA MATUKIO    MBALIMBALI KATIKA SIKU HIYO  TAREHE 10 DECEMBER 2011

 
PICHA YA PAMOJA YA WANASEDO


SAFARI IKAANZA
WANA-SEDO WALIPOWASILI IRENTE
  Ilichukua takribani muda wa dakika 45 wana SEDO hao kutoka SEKUCO wakawasili Irente Children`s  Home Na Ratiba ikafuata mkondo....................................

      
VIONGOZI WA SEDO WAKIPATA MAELEKEZO
Baada ya maelezo na ukaribisho wa awali kutoka kwa viongozi wa Irente Children`s Home pia kulikuwa na ukaribisho kutoka kwa Bi, Joyce Kibanga ambaye ni mkurugenzi wa huduma za jamii wilayani Lushoto.................taratibu za ukaribisho ziliendelea pale ambapo wana-SEDO walikunywa chai ya pamoja kituoni hapo!     



 
CHAI KWA PAMOJA
Mrs Joyce Kibanga, mkurugenzi.
 Wakati wana SEDO wakiendelea kunywa chai ya pamoja, historia fupi ya kituo hicho ilitolewa na Kiongozi wa kituo hicho. Walieleza madhumuni  na malengo ya kituo chao, ikiwa ni pamoja na kuwasaidia watoto waliopo kwenye mazingira magumu.




Wana SEDO wakifuatilia kwa makini Historia ya Irente Children`s Home
BAADAE WANA-SEDO HAO WALIKABIDHI MICHANGO YAO..............

Mwenyekiti wa SEDO, ROBERT SENTONGO, akikabidhi mchango.

 WANA SEDO BAADA YA KUKABIDHI ZAWADI-chini kulia ni the GREAT, chini kushoto ni Kaseka ( producers)

MWENEZI WA SEDO Frank Charles AKITOA MCHANGO











Baadhi ya wanachama wa SEDO wakipita kwa foleni kukabidhi michango yao ya Dhati kwa watoto wa kituo hicho.



BAADA YA WANA-SEDO KUKABIDHI MICHANGO YAO, HATUA ILIYOFUTA WALIELEKEA KWENYE KAZI MBALIMBALI KITUONI HAPO, IKIWA KAMA MCHANGO WA NGUVU KAZI.




AKINA DADA WA SEDO WAKIOSHA VYOMBO................................




TUMSIFU THE GREAT AKIPASUA KUNI.
MWENYEKITI WA SEDO AKIOSHA VYOMBO
the GREAT NA Deogratius WAKIOSHA
 VYOMBO.














MUDA ILIPOFIKA, WANASEDO WALIPATA NAFASI YA KUWAONA WATOTO KITUONI HAPO........................
PICHA YA PAMOJA NA WATOTO





ISMAIL(manager) akimsalimia mtoto kasimu
 PRODUCER K. AKISHOW LOVE KWA MAKIDS!
FRANK MAPALILO NAE HAKUWA NYUMA
PATRICK KITIGWA ( MR SEKUCO 2010-2011) AKIWA NA MTOTO HAPPY.......



EDITED, PRODUCED,DIRECTED, ARRANGED BY:
 TUMSIFU KOMBE, the GREAT,
KASEKA MZUMBWE    K-star.
ISMAIL JAALAN  the MANAGER
THE GREAT PRODUCTION @ 2011































RIDER_DECEMBER OFFICIAL VIDEO, VIDEO DIRECTED BY TUMSIFU KOMBE THE GREAT

CHAZ MAVOKO-SONG KWAHERI, Video directed by Tumsifu the great films

wibiya widget

TUMSIFU THE GREAT © 2012.All Rights Reserved.Designed by Tumsifu Kombe Modified by Nicolaus Trac-0716 276 000 :ICT EXPERT Sponsored by: JIPANGE