JIONEE WAKE ZA WATU WALIVYOFANYIWA KITU MBAYA

Wanawake a.k.a mijimama ya nguvu, wakazi wa Vibandani mjini morogoro, wamezua timbwili baada ya kufanyiana tukio la aibu na la kihistoria.
Wanawake hao ambao baadhi walidaiwa kuwa ni wake za watu, walinaswa wakifanya shindano lisilo rasmi la kukata nyonga hadi kuvua nguo hadharani na baadaye kuanzishiana.
Awali, wanawake hao (majina hayakupatikana), walianza kucheza muziki wa mwambao ‘mdogo mdogo’ lakini kadiri muda ulivyosonga ndivyo walivyokuwa wakibadilisha staili ya ukataji wa mauno hadi kufikia hatua ya kuvuana nguo na kurushiana mateke.
Hata hivyo, mtiti huo ulitulizwa na baadhi ya watu wenye heshima zao ambapo waliwataka wanawake hao kusitisha zoezi hilo kwani lilikuwa linawaibisha wao na mwenye shughuli yake.